African Lyon yaomba kurudisha Dar mchezo dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2019
African Lyon yaomba kurudisha Dar mchezo dhidi ya Simba

Klabu ya African Lyon imeandika Barua kwa Bodi ya Ligi Kuu ikiomba mchezo wake dhidi ya Simba ambao umepangwa kupigwa Februari 19 katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, urejeshwe uwanja wa Taifa, Dar es salaam

Klabu hiyo inadai kupata hasara kwenye mchezo dhidi ya Yanga kutokana na gharama za usafiri, kambi pamoja na makato mengine

Uamuzi huo wa sasa unakwenda tofauti na sababu yao ya mwanzoni kuwa waliamua kuhamishia michezo yao (dhidi ya Simba na Yanga) jijini Arusha kutokana na kukosa mashabiki Dar

Hata hivyo TFF imekataa ombi hilo na mchezo huo utapigwa Arusha kama ulivyopangwa

Hiki kilichofanywa na African Lyon kama kingekubaliwa na TFF basi huenda timu nyingine zingechukua maamuzi kama hayo ya kuhamisha viwanja vyao ya nyumbani KIHOLELA

Ni sheria, kabla ya ligi kuanza kila timu inabainisha uwanja wake wa nyumbani itakaotumia, uwanja huo hukaguliwa na wahusika kisha kuidhinishwa

Ni jambo la kushangaza kwa ligi kuu ya Tanzania timu inaweza kuruhusiwa kubadili uwanja wake wakati wowote tena bila ya sababu za msingi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’