Napata mashaka na waamuzi 'hasa waamuzi wasaidizi' kama wanakuwa na elimu ya kutosha kuweza kusimamia sheria 17 za mchezo wa mpira wa miguu
Ukweli ni kwamba wamekuwa wakifanya makosa yaleyale kila mara licha ya makosa hayo kubainishwa na wadau
Waamuzi wasaidizi wengi hawafahamu sheria ya kuotea.
Yanga imekuwa timu inayoathirika zaidi na maamuzi yao kutokana na mabao yake mengi kuwa yanakataliwa kwa sababu ya 'offside' ambazo sio sahihi
TFF inapaswa kuhakikisha waamuzi wake wanazifahamu vyema sheria 17 za mpira wa miguu kabla ya kuwapa majukumu ya kusimamia mchezo
Muda si mrefu matukio haya yataanza kuwaingiza waamuzi matatani hasa pale wachezaji watakapokosa uvumilivu
Wakati ligi ikiwa imeingia kwenye mzunguuko wa lala salama, uvumilivu wa baadhi ya matukio utazidi kupungua sawa na umuhimu wa pointi unavyoongezeka