Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemtahadharisha Mwanachama maarufu wa klabu ya Yanga anayefahamika zaidi kwa jina la 'Jitu' kuwa atamshitaki Mahakamani kama ataendela kufanya uchocheziΒ na kumkashifu
Hivi karibuni Jitu akiwa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari alisema mashabiki wa Yanga watampiga mawe kocha Zahera kama hatamchezesha Beno Kakolanya kwenye mchezo dhidi ya Simba iwapo Yanga itafungwa.
Aidha Jitu aliendelea kusema Zahera amemkataa Beno kwa sababu anataka kumsaidia mlinda lango Klaus Kindoki ambaye ni nduguye kutoka Congo
Alisema uwezo wa Kindoki ni mdogo sana na ni bora akachukuliwa mkewe kudaka kwenye mchezo dhidi ya Simba kama Beno hatarudishwa
"Jitu simfahamu sijawahi kukutana nae mahali popote katika maisha yangu. Ameenda kufanya video kusema mambo ya ovyo, mambo ya upumbavu"
"Anasema Zahera yule tutampiga majiwe kama Simba anatupiga sababu hamchezeshi Beno Kakolanya. Ninamtahadharisha kwa mara ya mwisho naweza nikamfunga," amesema Zahera
Mara kwa mara Jitu amekuwa akiingia katika mgogoro na viongozi wa klabu ya Yanga
Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika mwaka jana, Jitu alitolewa katika mkutano chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kupinga baadhi ya ajenda za Mkutano
