Kikosi cha Yanga leo jioni kitashuka kwenye uwanja wa Namfua kuikabili Singida United katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Yanga ilitua mkoani Singida juzi usiku na jana jioni ilifanya mazoezi katika uwanja Namfua utakaotumika kwenye mchezo huo
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo ulipita, Yanga inahitaji kuibuka na ushindi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa kumi jioni
Kocha Mwinyi Zahera amesema atakifanyia mabadiliko kidogo kikosi chake ili kuhakikisha wanaweza kuondoka na alama zote tatu leo licha ya wachezaji wake kukabiliwa na uchovu wa safari na kucheza mechi mfululizo
ADVERTISE HERE