Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema atakifanyia mabadiliko kikosi chake katika mchezo wa kesho dhidi ya Singida United kutokana na uchovu wa wachezaji.
Mcongoman huyo amesema atalazimika kuwapumzisha baadhi ya wachezaji waliotumika kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Coastal Union.
"Tumecheza juzi, jana tumesafiri kwa saa 15 kuja Singida. Nitabadili kikosi kukabiliana na uchovu wa wachezaji ili tuweze kuwa na ushindani na uwezo wa kupata ushindi katika mchezo huo," amesema
Aidha Zahera ameshangazwa na umbali wa kutoka mkoani Tanga hadi Singida akikiri kuwa jana ndio ilikuwa siku yake ya kwanza kusafiri kwa masaa 15 kwenda kucheza mechi
Yanga itasafiri tena umbali huo huo kurudi jijini Tanga kuikabili JKT Tanzania Februari 09 2019.
ADVERTISE HERE