Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema waamuzi wengi wanaochezesha ligi kuu hawajui kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu na wanachangia kudumaza soka nchini
Zahera amesema timu zinatumia gharama kusafiri mikoani lakini inasikitisha kuona waamuzi wanaharibu mechi kwa kufanya maamuzi ya hovyo
Amesema kwa aina ya waamuzi wanaotumiwa na TFF soka la Tanzania haliwezi kuendelea
"Kesho tutakwenda Singida tutatumia saa nane. Tutatoka Singida kurudi Tanga tutatumia saa nane. Tunalipa gharama za usafiri chakula, tunaingia uwanjani mtu mmoja anaharibu mchezo, Hivi kwa nini TFF na Bodi ya ligi wanaacha mambo haya yaendelee?," alihoji Zahera
"Namna hii mnataka soka la Tanzania liendelee? haiwezekani"
Zahera amesema anaamini Yanga ingeweza kuibuka na ushindi leo kama waamuzi wasingefanya mambo ya hovyo.
"Uwanja haukuwa tatizo kwetu. Tumekuwa tukicheza katika mazingira haya haya na kupata ushindi kwenye michezo kadhaa iliyopita. Tatizo ni uamuzi mbovu"