Watani zetu wamefungwa mabao 10 katika michezo miwili iliyopita ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Licha ya tambo za kuwa timu yenye pesa na kikosi kipana, aibu imewakumba na hakika wameiaibisha Tanzania kwani nadhani ndio timu ya kwanza kufungwa 5-0, 5-0 (mtawalia) katika michuano ya Afrika
Enzi za Manji sote tunakumbuka jinsi Yanga ilivyokuwa. Hao hao Al Ahly waliowapiga mkono jana, walinusurika kuondoshwa na Yanga katika michuano hiyo, walishukuru mikwaju ya penati
Yanga ilicheza na Al Ahly iliyokamilika na ikawalazimisha waarabu hao sare ya bao 1-1 katika dimba lao hilo hilo walilompigia mkono 5imba
Wakati huo Yanga ilikuwa na uwezo wa kusajili wachezaji bora.Ndio wakati ambao walikuja akina Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Obrey Chirwa. Kipindi hicho Haruna Niyonzima ndiye hasa, sio huyu feki tuliyewauzia
Jana 5imba walicheza na Al Ahly dhaifu iliyowakosa wachezaji tisa waliokuwa majeruhi
Wana Jangwani tuna nafasi ya kuirejesha Yanga mahali pake msimu ujao. Tumpe uwezo Kocha Mwinyi Zahera atutengenezee kikosi cha maangamizi kitakachoweza kuirudisha hadhi ya Tanzania kwenye michuano hiyo
Tuidhamini timu yetu wakati huu ambao bado tunajipanga kwenda kwenye uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya watakaoweka misingi imara ya Yanga kujitegemea
CHANGIA TIMU YAKO IKUPE FURAHA...