Kiungo wa Yanga Mohammed Issa 'Banka' ataanza kuitumikia timu hiyo Februari 10 itakapochuana na JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa dimba la Mkwakwani
Banka ambaye adhabu yake inamalizika Februari 08, amejumuishwa katika kikosi cha Yanga ambacho kimeelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union na kisha kuelekea mkoani Singida kuikabili Singida United
Banka atakuwa huru kuitumikia Yanga kwenye michezo ya ligi na kombe la FA baada ya Februari 08
Moja ya michezo muhimu ambayo kiungo huyo huenda akapata nafasi ya kuonyesha ufundi wake ni mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Februari 16 2019
Yanga ilimsajili Banka kutoka klabu ya Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka mitatu
Hata hivyo baadae ilibainika kuwa mchezaji huyo alikuwa amefungiwa miezi 14 na CAF baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo aliisaidia Zanzibar Heroes kucheza fainali ya michuano hiyo.