Kiungo Stand United ahojiwa na Uhamiaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2019
Kiungo Stand United ahojiwa na Uhamiaji

Kiungo wa Stand United Afidh Mussa ambaye inaelezwa uraia wake una utata, amehojiwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga na kutakiwa asiondoke nje ya mkoani huo wakati uchunguzi wa suala lake ukiendelea

Yanga imepeleka malalamiko TFF ikipinga mchezaji huyo anayedaiwa kuwa raia wa Burundi kusajiliwa na Stand United kama Mtanzania

Afidh alicheza katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Stand United dhidi ya Yanga uliomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Licha ya kuzaliwa nchini Tanzania, inadaiwa Afidh ana uraia wa Burundi

Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Yanga imenasa vielelezo vinavyothibitisha kiungo huyo kuwa na uraia wa Burundi

Moja ya vielelezo hivyo ni leseni ya mchezaji huyo aliyoitumia mwaka 2017 katika ligi kuu ya Burundi iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini humo likimtambua Afidh kuwa raia wa Burundi

Katika leseni hiyo iliyotolewa Septemba 14 2017, Afidh anatumia jina la Hererimana Afizi Mussa. Ametambulishwa kama raia wa Burundi anayetokea eneo la Cibitoke

Wakati katika klabu ya Stand United kiungo huyo anatambulika kwa jina la Afidh Mussa akiwa amesajiliwa kama Mtanzania leseni yake ikiwa namba 000238M93

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’