Mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo ambaye aliibuka kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi Disemba 2018, leo amekabidhiwa tuzo yake na wadhamini , kampuni ya BIKOSPORTS
Makambo amekabidhiwa tuzo hiyo na mwakilishi wa BIKOSPORTS Jeff Lea
Tuzo hiyo inakwenda sambamba na kukabidhiwa kitita cha fedha taslimu Tsh Milioni Moja
Nae kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye alishinda tuzo ya kocha bora kwa mara ya tatu msimu huu, alikabidhiwa zawadi kama hiyo na wadhamini kampuni ya BikoSports

ADVERTISE HERE