Mlinda lango wa Mbao Fc Metacha Mnata aliibuka kuwa kipa bora wa michuano ya SportPesa Cup akiisaidia Mbao kumaliza nafasi ya nne ya michuano hiyo
Metacha aliibeba Mbao Fc ilipoiondoa Gor Mahia kwa mikwaju ya penati kisha akaibuka nyota wa mchezo Mbao ilipocheza na Simba katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu
Bila shaka kocha Mwinyi Zahera na uongozi wa Yanga kwa ujumla wamemuona mlinda lango huyu
Badala ya kutumia gharama kubwa kuhangaika na magolikipa kutoka nje ambao uwezo wao unakuwa chini au hautofautiani na waliopo, ni bora kuwasajili hawa akina Metacha
Youthe Rostand na Klaus Kindoki wawafungua macho viongozi wa Yanga kuwa hakuna haja ya kutafuta walinda lango nje ya nchi, hapa nchini wako walinda lango wazuri sana
Wakati wa usajili wa dirisha dogo, iliripotiwa Yanga ilikaribia kumsajili mlinda lango wa Bandari Fc Farouq Shikalo ambaye timu yake ilicheza fainali ya SportPesa Cup na kufungwa bao 1-0 na Kariobang Sharks.
Hata hivyo mlinda lango huyo alitaka malipo makubwa hali iliyopelekea usajili wake kushindikana dakika za majeruhi
Lakini pengine dau hilo alilotaka (Mil 80) hapa hapa nchini Yanga ingeweza kusajili makipa hata watatu