Beki Hassani Kessy anayechezea Nkana Fc na kocha George Lwandamina wa ZESCO United juzi timu zao zilikutana katika mchezo wa ngao ya Jamii, Nkana ikishinda kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1
Msimu uliopita wawili hao walikuwa pamoja katika kikosi cha Yanga kilichotinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Wakati Lwandamina alivunja mkataba wake na kurudi ZESCO, Kessy aliondoka kujiunga na Nkana baada ya kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga kuhusu kusaini mkataba mpya
Nkana na ZESCO zote zimetinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho. Zimepangwa kundi moja, Feb 03 zitachuana katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
ADVERTISE HERE