Zahera atimiza ahadi, kampeni ya WanaYanga kuiendesha timu yao yaandaliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2019
Zahera atimiza ahadi, kampeni ya WanaYanga kuiendesha timu yao yaandaliwa

Mwanzoni mwa mwaka huu wakati akihojiwa katika kipindi cha Nyundo ya Baruani, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema atashirikiana na viongozi wa timu hiyo kuhakikisha wanaandaa utaratibu mzuri wa kuwashirikisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuiendesha timu yao

Zahera alisema Yanga ina utajiri mkubwa wa watu ambao kama wakitengenezewa utaratibu mzuri wataweza kuiendesha timu hiyo bila kutegemea wadhamini

Zahera kwa kushirikiana na viongozi wa Yanga wamebuni utaratibu wa kuichangia Yanga kupitia benki ya CRDB pamoja na mitandao ya simu.

Amesema utaratibu huo utawawezesha wadau wa Yanga kuichangia timu yao huku mapato yanayopatikana yakitangazwa kila wiki

Zahera amesema kuwa wako katika hatua za mwisho kufungua akaunti hiyo maalum ambayo 'signatories' wake atakuwa yeye Mwinyi Zahera, Ibrahim Ajib na Hafidh Saleh.

Zahera amesema atakuwa wa kwanza kuchangia kiasi cha Tsh Milioni Moja

Aidha tayari matangazo kuhusu kampeni hiyo yanaandaliwa Azam TV na kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kuanza kwa zoezi hilo

"Yanga ni timu tajiri ila haina mfumo mzuri wa kuwaweka pamoja wanachama wake na wakaweza kuigharamia timu yao," amesema Zahera

"Nimekuwa nikipita mahali watu wananipongeza kwa kazi nzuri wanaenda mbali zaidi wakielezea jinsi wanavoipenda timu yao na wapo tayari kuichangia

"Kwa hesabu za haraka Yanga ina mashabiki zaidi ya milioni 5 . Ukijenga utaratibu mzuri hao wanachama wakachangia 2500 tu kwa mwezi ni sawa na 12,500,000,000. Utasemaje timu maskini?

"Hiyo hela inatosha kusajili wachezaji piaΒ  kuwa na uwanja wetu.Β  Ili kuonesha tumedhamiria ndio maana tumefika hapa studio nikiwa na wachezaji saba, Cannavaro , Hafidh na katibu Omar Kaya. Tunaanda tangazo wiki ijayo litaanza kuruka hewani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’