Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini keshokutwa Jumanne Hotel ya Nefaland kujiandaa na mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Biashara United utakaopigwa Alhamisi, Januari 31, 2019
Vinara hao wa ligi kuu wamepania kushinda mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa
Katika hatua nyingine, mlinda lango Ramadhani Kabwili amepona majeraha na yuko tayari kwa ajili ya mchezo huo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga mapema leo, Kabwili atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoingia kambini
Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa viungo Raphael Daudi na Juma Mahadhi wameanza mazoezi mepesi baada ya kupona majeraha yaliyowaweka nje kwa muda mrefu
Mchezaji ambaye bado ni majeruhi ni winga Baruani Akilimali
ADVERTISE HERE