Ratiba ya Yanga ya ligi kuu ya Tanzania Bara inaonyesha baada ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United utakaopigwa Januari 31, mabingwa hao wa kihistoria wataelekea mkoani Tanga kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara ambao utapigwa Februari 03, dimba la Mkwakwani
Februari 06 Yanga itaelekea mkoani Singida kuikabili Singida United halafu siku tatu baadae inatakiwa kurudi tena jijini Tanga kuikabili JKT Tanzania Februari 09
Nadhani Bodi ya ligi inapaswa iingalie vizuri ratiba hii kwani Yanga ingeweza kucheza michezo yake yote miwili ya mkoani Tanga kisha kuelekea Singida.
Wakati huu ambao ligi haina mdhamini, na wakati huo huo timu mgeni ikiwa haiambulii chochote ugenini, si vyema kuziongezea gharama timu pasipo na sababu za msingi