Tatizo la Yanga liko hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2017
Tatizo la Yanga liko hapa
Makala hii ni kwa hisani ya Mwanaspoti, imaendikwa na Khatimu Naheka

Watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga juzi Jumapili ilicheza mchezo wa kwanza wa msimu wa 2017-2018 na kupata pointi moja dhidi ya Lipuli Iringa. Sio ajabu sana, lakini namna Yanga yenye kikosi chenye nyota wa kimataifa ilivyohenyeka ndipo inapoleta shida.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam na ulikuwa mgumu mno kutokana na mambo mengi ikiwamo maamuzi tata ya marefa, lakini kubwa udhaifu wa Yanga.

Lipuli ambayo imepanda Ligi Kuu msimu huu ilionekana kuivimbia Yanga na kuanza kufunga bao ambalo lilisawazishwa na Yanga.

Viongozi na mashabiki wa Yanga wanapaswa kuachana na mapungufu ya refa na badala yake kujikita katika kutafuta suluhisho lililopo ndani ya kikosi chao ambayo Mwanaspoti limeyainisha hapa chini.

SAFU YA USHAMBULIAJI

Safu hiyo imeyumba licha ya kuundwa na nyota wasiopungua saba akiwamo; Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Emmanuel Martin,

Obrey Chirwa, Juma Mahadhi, Matheo Anthony, Geofrey Mwashiuya na Ibrahim Ajibu.

Katika idadi ya nyota hao mpaka sasa watatu ni majeruhi ambao ni Mwashiuya, Tambwe na Chirwa.

Katika namna ya ajabu ni kwamba majeruhi hao wote wana tatizo la aina moja.

TAMBWE NA CHIRWA

Tambwe ni aina ya mshambuliaji ambaye huwa hatoki katika 18 ya timu pinzani. Na aina yake hii imempa faida ya kufunga kila mara.

Chirwa naye amekuwa na ubora kama huo kutokana na kutumia akili ya kulazimisha anapotaka kutafuta bao. Mara nyingi huwalazimisha mabeki kuingia nao ndani ya boksi. Ubora ambao umekuwa ukimpa nafasi ya kuwasumbua mabeki.

AJIBU NA NGOMA

Safu ya Yanga kwa sasa inawategemea Ngoma na Ajibu ambao sayansi inaonyesha kuwachezesha wawili hao kuna ugumu wa Yanga kupata mabao mengi kama inavyohitaji.

Inaonyesha wawili hawa asili yao ni washambuliaji wanaotakiwa kucheza nyuma ya mshambuliaji wa kati ambaye ana uwezo wa kusimama na kusumbuana na mabeki.

Ukiwafuatilia Ngona na Ajibu utaona wanatumia muda mwingi kushuka chini kitu ambacho kimekuwa kikiwapa nafasi mabeki kuwakaba kirahisi.

Ngoma na Ajibu wamekuwa wakitumia muda mwingi kuzunguka wakikosa mtu ambaye alitakiwa kusimama mbele yao na kuwapa msaada ili kutengeneza nafasi za mabao zinazoweza kupatikana kirahisi.

Watakapopatikana Chirwa na Tambwe hii itampa nafasi Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kuangalia sasa ni yupi aanze na yupi ili kuwa na safu bora yenye makali yanayoweza kuzalisha mabao kwani hii ya sasa imefeli kirahisi.

NAMBA HAZIDANGANYI

Ukiangalia msimu uliopita Yanga ilimkosa Ngoma kwa muda mrefu, ingawa alikuwa ameifungia mabao manane, lakini uwepo kwa Tambwe na Chirwa ulikuwa na faida kubwa kwa umahiri wao wa kufumania nyavu kwa aina ya soka wanalocheza.

Chirwa alimaliza akiwa na mabao 12, Tambwe akiwa na 11 na kuonyesha namna gani mastraika hao wanahitajika haraka kikosini kwa sasa kabla ligi haijachanganya, kwani wakiendelea kusalia nje itazidi kuigharimu Yanga kama ilivyobanwa na Lipuli.

Maana yake ni kwamba inawezekana Yanga ikamkosa Ngoma, kisha ikapata ubingwa lakini sio kuwakosa Tambwe na Chirwa waliounganisha nguvu kubwa na Simon Msuva kuibeba Yanga katika mechi za mwishoni mwa msimu uliopita.

Sio kama Ngoma na Ajibu hawana umuhimu lakini wanaweza kuwa mahiri zaidi wakicheza na mmoja kati ya Tambwe au Chirwa, kwa sababu watakuwa na kazi rahisi ya kutengeneza nafasi na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani na Yanga kupata ushindi kirahisi.

HAKUNA MBADALA NJE

Kama haijui Yanga haina wachezaji wa akiba kwa safu ya mbele katika benchi lake. Hakuna mbadala sahihi wa kuchukua nafasi ya mastraika wanaoanza kikosi cha kwanza.

Ni vigumu kumtegemea Anthony Matheo kuleta tija kumpokea Ngoma ama Ajibu, na siyo Matheo tu hata wengine wanaoanzia benchi ni muhali kuleta matokeo chanya kwa sababu hawajawahi kuwa Γ’β‚¬Λœsuper subÒ€ℒ.

Kama kungekuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama kina Chirwa na Tambwe katika benchi ni rahisi kuleta matokeo hata pale kina Ajibu na Ngoma wanapochemsha, hivyo kumsaidia Kocha Lwandamina katika kibarua chake Yanga.

Ndio maana nimewakumbusha Yanga waachane kabisa ya kumnyooshea kidole mwamuzi wa mechi ya Lipuli, badala yake wajiangalie wenyewe kipi kinachowakwaza kisha kuchukua hatua mapema kabla jahazi halijazama.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’