Mafanikio anayopata mshambuliaji Heritier Makambo hapa nchini yanavuma mpaka huko kwao Congo ambapo mdogo wa mshambuliaji huyo amesema hawatafurahi kama ndugu yao hataibuka mfungaji bora wa lgi kuu ya Tanzania Bara
Ezekiel Makambo anayesomea udaktari amesema kama nduguye hataibuka kuwa mfungaji bora au atashindwa kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu basi hatakuwa na mapokezi mazuri atakaporejea kwao
“Najua anaongoza kwa ufungaji, nafahamu anajua kufunga lakini tofauti ni ndogo, anatakiwa kufunga zaidi ili awe mfungaji bora,” Ezekiel amenukuliwa na Mwanaspoti
“Akifunga zaidi ataisaidia Yanga kubeba ubingwa, lakini ajue kabisa kama asipotimiza hayo atarudi hapa kimya kimya lakini akifanikiwa kufanya vyema basi hata mapokezi yatakuwa mazuri.”
Makambo anaongoza orodha ya wapachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 11 akifuatiwa na Eliud Ambokile wa Mbeya City mwenye mabao 10