Michezo ya raundi ya nne michuano ya kombe la FA (ASFC) ilianza kupigwa jana ambapo leo michezo sita imepigwa katika viwanja mbalimbali
Timu za ligi kuu KMC, Lipuli Fc, Kagera Sugar, Mbeya City na Alliance zimetinga raundi ya tano ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao ya leo
KMC imeifumua Pan African mabao 5-1 wakati Kagera Sugar imeshinda kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mbeya Kwanza
Polisi Tanzania nayo ikafungwa na Lipuli Fc kwa mikwaju ya penati 2-3 baada ya matokeo ya 1-1
Wababe wa Simba, Mashujaa Fc imelazwa bao 1-0 na Mbeya City na kutupwa nje ya michuano hiyo
Alliance Fc ikailaza La Familia 2-0 wakati Dodoma Fc inayonolewa na Jamhuri Kiwhelo 'Julio' imepenya raundi ya tano kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Transit Camp
Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wao watashuka dimbani Alhamisi ijayo kuikabili Biashara United