Ajib atatambulishwa mkataba wake na Simba utakapokwisha

Admin By Admin
β€’
21 Jun 2017
Ajib atatambulishwa mkataba wake na Simba utakapokwisha
Kuna watu hawaamini kuwa baadhi ya wachezaji wanaodaiwa kusajiliwa na Yanga ni uzushi kwa kuwa hawajaonekana wakitambulishwa kama ilivyokuwa kwa yule beki aliyetoka Jan'gombe, Shaibu.

Ukweli ni kwamba baada ya makosa yaliyofanywa msimu uliopita kwa kumtambulisha Hassan Kessy siku mbili kabla mkataba wake haujamalizika, msimu huu mambo hayo hayatakiwi kutokea.

Uzembe uliofanywa msimu uliopita ulipelekea Yanga kuilipa Simba Mil 50 kwa mchezaji ambaye alipaswa kusajiliwa bure kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umemalizika.

Sasa swala la Ibrahim Ajib liko hivyo. Mkataba wa Ajib na Simba utamalizika mwishoni mwa mwezi huu. Hivyo hawezi kuwekwa hadharani kabla ya muda huo.

Yanga itawatambulisha wachezaji wote wapya pale mikataba yao na timu zao za zamani itakapokuwa imekamilika.

Hata kwa watani zetu Simba, wamemsajili Aishi Manula lakini hawajamtambulisha popote naye ni kwa sababu mkataba wake na Azam FC bado una siku kadhaa kabla ya kumalizika kabisa.

AJIB ALIKOIBUKIA

Ajib ni mchezaji aliyeibukia timu ya vijana ya Simba, ambayo ilimtoa Boom FC ya Ilala mwaka 2013, lakini baadaye akaondoka kwenda kujikomaza kwenye timu ambazo angepata nafasi ya kucheza.

Alichezea Mwadui FC na kuisaida kupanda Ligi Kuu msimu wa 2014-2015.

Alikuwa na mwanzo mzuri Simba SC chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic na nyota yake kidogo iliendelea kung'ara chini ya kocha Muingereza, Dylan Kerr ingawa baada ya ujio wa Mganda Jackson Mayanja na baadaye Mcameroon, Joseph Marius Omog mambo yakaanza kuwa tofauti kidogo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’