Kikosi cha Yanga leo kimejifua katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Biashara Fc utakaopigwa Januari 31, 2019
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa mchezo huo utapigwa Januari 31 na sio 29 kama ilivyotaarifiwa awali
Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya SportPesa juzi, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja na leo wameanza kujifua kujiandaa na mchezo huo ambao ni matokeo ya ushindi pekee ndio yataihakikishia Yanga kusonga mbele hatua ya 16 bora
ADVERTISE HERE