Mabingwa watetezi wa michuano ya SportPesa Cup kwa misimu miwili mfululizo Gor Mahia wameondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa na Mbao Fc kwa mikwaju ya penati
Mbao Fc imeshinda kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1
Mkongwe Denis Oliechi aliifungia bao la kuongoza Gor Mahia kwenye kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penati kabla Abubakary Ngalema hajaisawazishia Mbao kwenye dakika ya 76
Ushindi huo wa Mbao umepunguza utawala wa timu za Kenya kwenye michuano hiyo
Mpaka sasa timu mbili kutoka Kenya, Bandari Fc na K Sharks zimetinga nusu fainali na Mbao Fc imekuwa timu kwanza kutoka Tanzania kutinga hatua hiyo
ADVERTISE HERE