Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ameipa kipaumbele michuano ya SportPesa Super inayoanza kesho jijini Dar es salaam
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho ambapo Yanga itachuana na K Sharks, Zahera amesema amefurahishwa na maandalizi yaliyofanywa na kampuni ya SportPesa na ameahidi Yanga itawapa burudani mashabiki wake
Zahera amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanafanya vizuri lengo kuu likiwa kutwaa ubingwa
"Nawaambia mashabiki wetu waje kwa wingi kesho uwanjani kwani tumejiandaa kuwapa burudani. Tumejiandaa kikamilifu kufanya vizuri kwenye mashindano haya," amesema Zahera
"Nitatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza. Mwanzoni mwa msimu niliweka malengo matatu ambayo ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la SportPesa na Kombe la FA (ASFC). Tutashiriki michuano hii tukiwa tumekamilika"
Nae nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema wachezaji wa timu hiyo wako tayari kwa ajili ya mashindano hayo huku akiahidi kuwa wamepania kucheza fainali za michuano hiyo mwaka huu