Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wamerejea jijini Dar es salaam jana wakitokea mkoani Shinyanga walikomenyana na Stand United katika mchezo wa ligi uliomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Baada ya kuwasili, Yanga ilielekea moja kwa moja kambini kujiwinda na mchezo wa robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup utakaopigwa kesho dimba la Taifa dhidi ya KK Sharks saa 10:15 jioni
Yanga imeipa kipaumbele michuano ya SportPesa ya mwaka huu ambapo imejiwekea malengo ya kutwaa ubingwa utakaowahakikishia fedha taslim karibu Milioni sabini pia kukata tiketi ya kuchuana na Everton
ADVERTISE HERE