Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu kwa kufungwa bao 1-0 na Stand United mkoani Shinyanga leo
Ni matokeo ambao hayawapendezi Wana Jangwani lakini ndio mpira ulivyo, kuna wakati wa furaha na upo wakati wa huzuni pia
Yanga imefungwa katika mchezo wake wa 20, kimsingi wachezaji na benchi la ufundi bado wanastahili pongezi kwa kazi kubwa waliyofanya
Kucheza mzunguuko wote wa kwanza bila ya kufungwa licha ya changamoto zinazowakabili mabingwa hao wa kihistoria ni mafanikio makubwa
Kutunza rekodi ya kutofungwa sio jambo rahisi na ndio maana ni timu chache sana duniani zilizowahi kucheza msimu mzima bila kufungwa
Yanga isichukulie matokeo haya kama ni kushindwa, bali wayatumie kujiimarisha ili kuweza kufanya vizuri katika michezo ijayo
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza Jumanne ijayo ambapo Yanga itashuka dimbani kuchuana na K Sharks.
K Sharks kutoka nchini Kenya tayari imewasili jijini Dar es salaam