Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amepitishwa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya ligi TPBL sambamba na Ahmed Yahya.
Leo Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mbali na nafasi ya Mwenyekiti, Shan Crysostoms amepitishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti.
Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.
Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

ADVERTISE HERE