Kinara wa mabao ligi kuu ya Tanzania Bara Heritier Makambo ataongoza kikosi cha Yanga kuikabili Stand United kesho kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa dimba la Kambarage
Makambo aliyetua hivi karibuni kutoka Congo, yuko Shinyanga na kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania
Baada ya kukosa mchezo uliopita dhidi ya Mwadui Fc, Makambo amepania kuwaadhibu Stand United ili kujiongezea mabao katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Mcongomani huyo mwenye mabao 11 amekuwa gumzo zaidi miongoni mwa mashabiki wa Yanga hapa Shinyanga
Yanga iliwasili mkoani Shinyanga ikitokea Mwanza ilikotua kwa usafiri wa ndege mapema asubuhi
Leo itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Kambarage tayari kwa mchezo hapo kesho
ADVERTISE HERE