Uongozi wa Klabu ya Yanga unasikitika kutangaza kifo wa mchezaji wake wa zamani Hassan Gobos aliyefariki jijini Dar es salaam.
Msiba wa mkongwe huyo upo nyumbani kwake Sinza Mori na mazishi yatafanyika kesho Ijumaa Alasiri katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Gobos aliwahi kuitumikia Yanga kwa mafanikio kuanzia miaka ya 60 hadi mwishoni mwa miaka ya 70 akipata nafasi ya kuitumikia timu ya Taifa pia
Ni miongoni mwa wachezaji waliotamba sana kwenye kikosi cha Yanga wakati huo.
Inna lillahi wainna ilaihi raajiun..
ADVERTISE HERE