Wakati mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Mwadui Fc ukiendelea jana katika dimba la Taifa, utaratibu wa kupitisha 'bakuli' kwa mashabiki kuichangia timu yao ulikuwa ukiendelea
Utaratibu huo ambao sasa umekuwa rasmi na unaendeshwa na mashabiki wa Yanga katika kila mchezo ambao timu hiyo inashuka dimbani, ulifanikisha kupatikana kwa fedha taslim Shilingi laki saba
Fedha hizo zilikabidhiwa kwa nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul baada ya mchezo huo.
Moja ya mambo yanayoifanya Yanga ifanikiwe wakati huu licha ya kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, ni umoja uliopo kati ya viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo
Wana Yanga wameikubali hali ya timu yao kwa sasa na wameamua kuchukua hatua kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
Kwa hili wanastahili pongezi. Hii ndio maana halisi ya timu ya Wananchi