Wakati ligi kuu ya Tanzania Bara ikiingia mzunguuko wa 22, Simba huenda ikavunja rekodi ya kuwa na viporo vingi msimu huu ikiwa imeshuka dimbani mara 14 tu
Ni jambo la kushangaza Bodi ya Ligi Kuu kuruhusu timu hiyo kuwa na idadi kubwa ya viporo kwa kisingizio kuwa inashiriki michuano ya CAF ilihali mambo kama hayo hayapo nchi nyingine ambazo pia zinashiriki michuano hiyo.
Kundi D ambalo Simba ipo sambamba na Al Ahly, AS Vita na JS Saoura, ukiondoa Misri,Β ligi za Congo na Algeria zimeendelea kama kawaida kwa timu zao kucheza michezo yao sambamba na michezo ya ligi ya mabingwa
Ni ligi kuu ya Misri pekee ambayo Al Ahly ina viporo vinne, kwa nchi nyingine timu zote zina michezo karibu sawa.
MISRI

CONGO DR

ALGERIA

TANZANIA

Kwa hali ilivyo mpaka kufikia mwanzoni mwa mwezi wa pili huenda Simba ikakusanya michezo ya kiporo isiyopungua 10!
Hiyo inaweza kuwa rekodi ya dunia
Yanga imeshiriki michuano ya CAF mara nyingi lakini sikumbuki wakati ambao ilikuwa na michezo ya kiporo zaidi ya mitano
Misimu miwili iliyopita Simba iliwahi kuomba kusimamishwa michezo yake hadi pale Yanga itakapocheza michezo yake yote ya viporo
Lakini hali ni tofauti kwa msimu huu ambao uongozi wa Simba umeonekana kuridhika 'kurundikiwa' viporo
Aidha Yanga haionekani 'kushughulishwa' na viporo hivyo vya Simba kwani imeendelea kushinda michezo yake na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya Azam fc na alama 20 dhidi ya Simba
Hata kama Simba itashinda michezo yote ya viporo Yanga itandelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tano