Mshambuliaji wa Yanga Mcongomani Heritier Makambo amewasili nchini usiku wa kuamkia leo akitokea kwao DR Congo alikokwenda kwa ajili ya mapumziko
Baada ya kutua nchini, moja kwa moja Makamo ameungana na kikosi cha Yanga ambacho kinajiandaa na safari ya mkoani Shinyanga kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Jumamosi, Januari 19 2019

Mkali huyo wa kuzifumainia nyavu aliyefunga mabao 11 mpaka sasa, amemaliza uvumi uliokuwa umetawala kuwa asingerudi katika klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE