Kiungo Pius Buswita, amekiri kusaini mikataba miwili kwenye vilabu viwili tofauti katika msimu mmoja akitokea Mbao FC ya Mwanza, hatua ambayo imemsababishia rungu la kufungiwa mwaka mmoja na TFF.
Buswita amekiri kufanya kosa hilo kupitia kwa wakala wake Medi Mtabora huku akieleza sababu kuwa ni kupitiwa na shetani baada ya kubanwa na wahusika waliomsainisha mkataba wa pili.
"Mkataba ninaoutambua ni wa Yanga, nimehusika katika hatua zote kumpeleka Yanga, sasa nashangaa haya yametoka wapi," amesema Mtabora
"Mwenyewe nilipomuuliza amesema shetani alimpitia kwa kuwa hao watu walimbana sanaΓ’β¬Β amefunguka Mtabora wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ndiyo iliyobaini kuwa Buswita amesaini mikataba ya klabu mbili tofauti katika msimu mmoja wa 2017/18.

ADVERTISE HERE