Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela leo anatarajiwa kuweka hadharani hatma ya uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga wa kujaza nafasi zilizowazi.
Uchaguzi huo uliopaswa kufanyika juzi Jumapili, Januari 13, uliahirishwa kufuatia baadhi ya Wanachama wa klabu ya Yanga kufungua kesi Mahakamani wakipinga mwenendo wa mchakato wake
Awali TFF iliahidi kutoa taarifa jana lakini ilishindwa kufanya hivyo.
Msemaji wa Tff Clifford Mario Ndimbo, amesema leo hii saa saba mchana Mchungahela ataelezea hatma ya mchakato wa uchaguzi huo
ADVERTISE HERE