Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo kinashuka katika dimba la Taifa kuikabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 22.
Yanga vinara wa ligi kuu watakuwa wanasaka ushindi wao wa kwanza mwaka huu kwenye ligi. Ushindi ambao utawaimarisha zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa moja usiku.
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A Tsh 15,000/-, VIP B na C Tsh 10,000/- na Mzunguuko Tsh 5,000/-
Makambo bado hajarudi
Yanga itashuka dimbani katika mchezo huo bila ya mshambuliaji wake kinara wa mabao Heritier Makambo ambaye bado hajarejea kutoka DR Congo alikokwenda kwa ajili ya mapumziko
Mkongwe Amissi Tambwe anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya vinara hao wa ligi kuu.
Aidha beki Andrew Vicent 'Dante' anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosa michezo minne kufuatia Kamati ya Nidhamu ya TFF kutompata na hatia kwenye tuhuma za kufanya matukio ya utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons