Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten ametoa ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa iliyoripotiwa mapema leo kuhusu mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo ambapo amethibitisha kuwa mshambuliaji huyo bado hajarejea kutoka DR Congo alikokuwa amekwenda kwa mapumziko
Ten amesema Makambo alipewa ruhusa na kocha Mwinyi Zahera kwenda kwao Congo kwa ajili ya mapumziko na alikuwa akiwasiliana na kocha huyo wakati wote aliokuwa huko
Hata hivyo tangu juzi Ten amesema imekuwa vigumu kuwasiliana na mshambuliaji huyo kwa kuwa hapatikani kwenye simu na wameshindwa kufahamu amekumbwa na tatizo gani.
"Kimsingi sio kweli kwamba Makambo ameondoka Yanga," amesema Ten
"Bali kumekuwa na changamoto ya mawasiliano katika siku mbili hizi, kocha amekuwa akimtafuta bila ya mafanikio"
"Ifahamike Makambo alipewa ruhusa ya kwenda kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko na wakati wote aliokuwa huko alikuwa akiwasiliana na kocha Zahera isipokuwa siku mbili hizi"
"Makambo ni mchezaji anayejielewa hawezi kuondoka kiholela tunaamini hata watu wake wanaomsimamia wanalifahamu hilo"
"Kilichotokea ni changamoto ya mawasiliano na tunafanya jitihada za kuwasiliana nae ili tufanye utaratibu wa yeye kurejea nchini kuendelea na majukumu yake," amesema