Manji atarudi Yanga kesho?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jan 2019
Manji atarudi Yanga kesho?

Baada ya wanachama wa Yanga kuzuia uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi uliokuwa umepangwa kufanyika jana, Januari 13 huenda Yusufu Manji akarejea katika nafasi ya Uwenyekiti wa klabu hiyo imefahamika.

Mwaka jana kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga, Wanachama waliikataa barua ya kujiuzulu ya Manji wakimtaka arejee katika nafasi yake.

Novemba 11, 2018 Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Yanga George Mkuchika aliwathibitishia WanaYanga uamuzi wa Manji kuridhia kurejea klabuni hapo akiwa tayari kuanza kazi Januari 15, 2019 kulingana na barua aliyoandika

Sasa kwa mujibu wa barua hiyo, Manji anapaswa kuripoti kazini na kuanza kazi rasmi siku ya kesho Jumanne

Baadhi ya Wanachama wa Yanga walikwenda Mahakamani kupinga uchaguzi mdogo wa klabu hiyo kusimamiwa na TFF wakitaka ufafanuzi wa Mahakama juu ya nani mwenye uhalali wa kusimamia uchaguzi huo

Aidha Wanachama hao wanataka Katiba ya Yanga iheshimiwe. Katiba hiyo inahalalisha Maamuzi yao kupitia vikao vyao rasmi.

Wakati hatma ya uchaguzi huo ikiwa gizani kutokana na zuio la Mahakama, ni dhahiri Yanga inahitaji kuwa na uongozi kamili wa kuweza kuisimamia klabu hiyo

Juzi Salum Mkemi mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alijiuzulu, alitangaza kurejea katika nafasi yake akidai barua yake ya kujiuzulu haikujibiwa

Mkemi aliongeza kuwa kwa sasa Kamati ya Utendaji pia haina uwezo wa kuijadili barua yake kutokana na kukosa sifa.

Uamuzi huo wa Mkemi unaweza kutengeneza mgogoro mwingine kwani nafasi yake ni miongoni mwa nafasi zilizotangazwa na TFF kuwa wazi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’