Kaaya lawamani usajili wa kipa mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jan 2019
Kaaya lawamani usajili wa kipa mpya

Jana nusura ziibuke vurugu Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam kufuatia wanachama wa klabu hiyo kumvaa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaaya wakimtuhumu juu ya masuala mbalimbali

Vurugu hizo zilichagizwa zaidi baada ya mwanachama mmoja kumtuhumu Kaaya kuhusika katika usajili wa mlinda lango Ibrahim Hamid aliyesajiliwa mwezi uliopita siku moja kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa.

Mwanachama huyo aliyekuwa na 'jazba' alimtuhumu Kaaya kushirikiana na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Hussein Nyika kukwamisha usajili wa wachezaji wapya kwa maslahi yao huku wakimsajili mlinda lango Hamid bila ya kumshirikisha kocha Mwinyi Zahera.

Zahera alimkana mlinda lango huyo akidai hakuwa akimfahamu na alishangaa ilikuwaje akasajiliwa bila ya idhini yake.

Hamid alionyesha kiwango cha chini kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo Yanga iliyopeleka timu ya vijana, ilitolewa kwenye hatua ya makundi.

Mashabiki wengi wameponda usajili wa mlinda lango huyo aliyesajiliwa akiwa mchezaji huru aliyetokea kucheza soka la ufukweni.

Tangu itangazwe taarifa ya kuahirishwa uchaguzi wa Yanga, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wamekuwa wakifurika Makao Makuu ya Yangawakitaka wapewe taarifa juu ya kinachoendelea klabuni hapo

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’