Klabu ya Yanga imepokea mgawo wa pili wa fedha Mil 600 wanazopaswa kulipwa na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) baada ya kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho ,msimu uliopita.
Inaelezwa Yanga imepokea kiasi cha Tsh Mil 300 ikiwa ni awamu ya pili baada ya kuwa tayari ilishapokea kiasi kama hicho cha fedha mwaka jana.
Kiasi hicho cha fedha kimepunguza madai ya wachezaji na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Mwinyi Zahera
Hii ni habari njema kwa vinara hao wa ligi kuu ya Tanzania Bara ambao msimu huu wamepania kurejesha ubingwa walioupoteza kwa watani zao Simba, msimu uliopita.
ADVERTISE HERE