Twende na Igangula au Dk Tiboroha?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2019
Twende na Igangula au Dk Tiboroha?

Wagombea wawili wa nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga Baraka Igangula na Dk Jonas Tiboroha leo watachuana katika mdahalo utakaorushwa mbashara na Azam Tv kuanzia saa tatu na nusu usiku kupitia chaneli ya Azam Sport 2.

Mdahalo huo pia utahusisha wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti

Igangula na Dk Tiboroha wanachuana vikali kwenye kampeni kuelekea uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi utakaofanyika keshokutwa Jumapili

Wote wamejipambanua kutaka kufanya mabadiliko ya kweli katika klabu ya Yanga

Wakati Igangula akijipambanua kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu na kuwashughulikia walioifisadi Yanga, Dk Toboroha yeye amejikita katika kushirikiana na kuirejesha timu kwa Wanachama.

Wagombea wote wameahidi kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga ili timu iweze kujiendesha kwa mfumo wa kisasa

Wote wameonyesha kukerwa na mfumo wa mauzo holela ya jezi za Yanga unaoikosesha klabu mapato na kuahidi kurekebisha hilo.

Wote ni wasomi, na wana uzoefu na uongozi wa Yanga kwani wamewahi kuwa viongozi wa Yanga kwa nyakati tofauti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’