Stars yaingia kambini tayari kwa mchezo dhidi ya Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
29 Aug 2017
Stars yaingia kambini tayari kwa mchezo dhidi ya Botswana
Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana, kimeanza mazoezi leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, huku nyota wanaocheza nje wakitarajiwa kuwasili kuanzia kesho.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema kwamba wachezaji wote wanaocheza hapa nchini waliingia kambini jana, huku wanaocheza nje wakitarajiwa kuwasili kuanzia kesho.

“Jana jioni wachezaji wa timu za Azam FC, Yanga pamoja na Simba SC waliingia kambini na kikubwa cha kwanza Daktari wa timu aliwapima afya zao leo asubuhi na jioni timu ikaanza mazoezi Uwanja wa Uhuru, “amesema.

Lucas amesema kwamba msafara wa wachezaji 18 na viongozi tisa kutoka Botswana unatarajiwa kuwasili Alhamisi kabla ya kufanya mazoezi katika Uwanja utakaotumika kawa mechi Ijumaa.

“Wenzetu tumewasiliana nao na wamesema watakuja na wachezaji 18 na viongozi tisa, tunazungumzia msafara wa watu 27 na timu itafika Agosti 31, lakini hatujajua ni muda gani watawasili,”amesema.

Lucas amesema wamekwishafanya mawasiliano na wachezaji wanaocheza nje walioitwa kujiunga na kikosi cha Stars akiwemo Nahodha, Mbwana Ally Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, Farid Mussa wa CD Tenerife ya Hispania, Simon Msuva wa Difaa Hassan El –Jadida ya Morocco na Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini na wote wanatarajiwa kuanza kuwasili kesho.

Kuhusu suala la Uwanja utakaotumika katika mechi hiyo Alfredy amesema, wamethibitisha Uwanja wa Taifa upo katika ukarabati ulioanza siku tano zilizopita na mchezo dhidi ya Botswana sasa ni rasmi utapingwa Uwanja wa Uhuru.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →