Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi ligi kuu ya Wanawake kati ya Yanga Princess dhidi ya Simba Queens utapigwa Jumapili, Januari 13 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam
Mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi Jumapili katika dimba la Karume kuwaunga mkono kinadada wa Yanga Princess waweze kuwaadhibu watani zao Simba Queens.
Kiingilio cha mchezo huo ni Tsh 2,000/- tu.
Mpaka sasa Yanga Princess imeshuka dimbani mara nne, imeshinda michezo miwili na kupoteza michezo miwili.
ADVERTISE HERE