Mlinda lango wa Malindi Fc Ahmed Ali Suleiman amekiri kufuatwa na viongozi wa Yanga ambapo walifanya mazungumzo kuhusu usajili
Suleiman maarufu kwa jina la 'Salula' amesema viongozi hao wa Yanga walimwambia kuwa wanataka kumsajili ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania
"Ni kweli nimefanya mazungumzo na viongozi wa Yanga wamesema wananihitaji," Salula aliiambia Dauda TV
Wakati hatma ya mlinda lango Beno Kakolanya ikiwa bado mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera, ni kama Yanga imeanza mchakato wa kusaka mlinda lango mwingine atakayechukua nafasi yake
Huenda Salula akatua Yanga mwezi Julai wakati wa usajili wa dirisha kubwa baada ya Ibrahim Hamid aliyesajiliwa mwezi uliopita wakati wa usajili wa dirisha dogo kushindwa kuonyesha makali.
ADVERTISE HERE