Kampeni za uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga zimezinduliwa rasmi jana ambapo wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza kupita katika matawi ya klabu hiyo kuwashawishi wanachama waweze kuwapigia kura.
Uchaguzi wa Yanga utafanyika Januari 13 2019 ambapo nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe Wanne wa Kamati ya Utendaji.
Jambo la msingi kwa wanachama wa klabu ya Yanga ni kujipa muda wa kuwasikilza wagombea wote, kuchuja sera zao kabla ya kufanya uamuzi siku ya uchaguzi.
Yanga iliyokumbwa na changamoto za kiuchumi inahitaji kupata viongozi watakaokuwa na mawazo na mipango madhubuti ya kutatua changamoto hizo na kuirudishia Yanga hadhi yake.
Huu ni wakati wa Wana Yanga kusahau tofauti zao na kushiriki uchaguzi huo ili kuwapata viongozi watakaopeleka mbele gurudumu la Yanga.
Wagombea wa nafasi ya Uwenyekiti ni Mbaraka Igangula na Dk Jonas Tiboroha wakati wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Yono Kevela, Titus Osoro na Salum Chota