Ratiba ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza Januari 22 mpaka Januari 27 2019 tayari imetolewa ambapo Yanga itanza na timu kutoka nchini Kenya K Sharks katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni uwanja wa Taifa.
Iwapo Yanga itashinda mchezo huo itatinga nusu fainali ambapo katika hatua hiyo itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Mbao Fc dhidi ya Gor Mahia.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajia kutumia kikosi chake kamili kwenye michuano hii ambayo bingwa atajinyakulia kombe na fedha taslim zaidi ya Mil 70
Aidha bingwa pia atapata nafasi ya kucheza na Everton inayoshiriki ligi ya Uingereza kwenye mchezo ambao utapigwa dimba la Taifa mwezi Julai 2019.

ADVERTISE HERE