Kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana na kujadili rufaa mbili zilizowasilishwa katika Kamati hiyo na Wagombea wa Uchaguzi wa Klabu ya Young Africans.
Rufaa zilizo jadiliwa ni ya Eng Leonard Marango ambaye hakuridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi na rufaa ya pili ilikuwa ya Yono Kevela ambaye naye alilalamika kutoridhishwa na maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi.
Kamati ilisikiliza utetezi wa warufani na Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambapo mrufani eng Leonard Marango alitoa utetezi wake kwamba hakufika kwenye usaili katika siku zillizopangwa kwasababu alisafiri na kuchelewa kufika kwa wakati.
Baada ya kusikiliza utetezi Kamati imejiridhisha kuwa mrufani alishindwa kuhudhuria usaili bila taarifa yoyote hivyo imetupilia mbali rufaa hiyo.
Mrufani wa pili Yono Kevela aliyelalamika maamuzi ya kuenguliwa jina lake kwenye majina ya wagombea Kamati ilipokea na kusikiliza utetezi wa mrufani na Kamati ya Uchaguzi.
Kamati imekubaliana na utetezi wa Yono Kevela na kumrudisha kuwa mmoja wa Wagombea katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Kamati hiyo ilikutana chini ya Mwenyekiti wake Keneth Mwenda.