Mashabiki wengi wa Yanga hawakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na mlinda lango mpya wa Yanga Ibrahim Hamid ambaye alisajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi uliopita.
Hamid ameruhusu mabao matano kwenye michuano hiyo jana 'akitunguliwa' mabao mawili kwa mashuti ya nje ya 18 na Malindi Fc
Michuano hii ilikuwa nafasi adim kwa Himid kuonyesha uwezo wake ili kuwanyamazisha wale waliokuwa wakikosoa usajili wake uliodaiwa kufanywa bila ya kocha Mwinyi Zahera kufahamu
Hata hivyo mkufunzi wa makipa Juma Pondamali ana kazi ya ziada kuimarisha kiwango cha mlinda lango huyo mrefu kabla ya kumtumia katika michuano mikubwa
ADVERTISE HERE