Yanga imeiaga michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kulazwa mabao 2-1 na Malindi katika mchezo uliopigwa dimba la Amaan Jumatatu jioni.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo wa Yanga ambayo mchezo uliopita ililazwa mabao 3-0 na Azam Fc.
Malindi imefikisha alama saba baada ya ushindi wa leo sawa na Azam Fc wakati Yanga yenye alama tatu hata ikishinda mchezo wake wa mwisho haitaweza kuzifikia timu hizo
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera hakuipa kipaumbele michuano hiyo ambapo aliwapa mapumziko wachezaji wake wa kikosi cha kwanza huku akituma timu ya vijana visiwani Zanzibar
Yanga imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Jamhuri Fc
ADVERTISE HERE