Msimu wa tatu wa michuano ya SportPesa Super Cup unatarajiwa kuanza Januari 22-27 2019 kwa michuano hiyo kupigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Awali michuano hiyo ilikuwa ifanyike mikoa ya Dar es salaam na Mwanza lakini sasa mkoa wa Mwanza hautahusika ambapo Mbao Fc iliyoalikwa kushiriki michuano hiyo itaungana na timu nyingine mkoani Dar es salaam.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha dola 30,000 (Zaidi ya Mil 68) na atapata nafasi ya kucheza na Everton, timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Mchezo dhidi ya Everton utapigwa jijini Dar es salaam mwezi Julai 2019 wakati wa maandalizi ya msimu mpya 2019/20.
ADVERTISE HERE