Kocha wa Azam Fc Hans van Pluijm ameendeleza ubabe wake dhidi Yanga, timu yake ya zamani baada ya leo kuiongoza Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kombe la mapinduzi, kundi B
Obrey Chirwa ameifungua Azam Fc mabao mawili leo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria tangu alipoondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Bao jingine la Azam Fc lilifungwa na Enock Atta kupitia mpira wa adhabu.
Kukosa uzoefu kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga kumeigharimu timu hiyo ambayo inatumia kikosi chake cha vijana na wazoefu watano katika michuano hiyo.
Matokeo hayo yameipelekea Azam Fc kileleni mwa kundi B baada ya kufikisha alama nne.
ADVERTISE HERE