Afisa Habari wa Yanga , Dismas Ten amesema uongozi umekuwa ukifuatilia swala la kiungo Pius Buswita aliyefungiwa mwaka mmoja na TFF akituhumiwa kusajiliwa na timu mbili, Simba na Yanga.
Kwenye taarifa aliyoitoa leo, Ten amesema swala lake liko mbioni kupatiwa ufumbuzi na huenda Buswita akaanza kuitumikia Yanga siku chache zijazo.
Aidha, Ten amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa sapoti waliyoitoa katika mchezo dhidi ya Lipuli ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Amesisitiza kuwa matokeo hayo hayataizuia Yanga kutwaa taji la nne mfululizo kutokana na ubora wa kikosi.
Amejulisha kwamba majeruhi Obrey Chirwa, Beno Kakolanya, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya wanaendelea vizuri na watarejea dimbani siku chache zijazo.

ADVERTISE HERE