Tuzo ya kocha bora Disemba wampe tu Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jan 2019
Tuzo ya kocha bora Disemba wampe tu Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ni kama anasubiri tu kukabidhiwa tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi Disemba 2018.

Zahera ambaye tayari ameitwaa tuzo hiyo mara mbili, (Septemba na Novemba), anaweza kuitwaa tena kutokana na mafanikio aliyopata na kikosi cha Yanga mwezi wa 12.

Katika mwezi huo Yanga ilicheza michezo mitano na kufanikiwa kushinda michezo yote. Ni Zahera pekee mwenye takwimu hizo za kibabe ukilinganisha na makocha wengine katika mwezi huo

Aidha washambuliaji Amissi Tambwe na Heritier Makambo wanaweza kuingia katika kinyan'ganyiro cha mchezaji bora wa mwezi huo baada ya kufanya vizuri.

Makambo aliiyeibuka mchezaji bora wa mwezi Novemba 2018, mwezi wa 12 ameifungia Yanga mabao manne na yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuitwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

Tambwe alifunga mabao matatu mwezi Disemba wakati beki Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyewania tuzo ya mwezi Novemba, ameifungia Yanga mabao mawili mwezi Disemba.

Tuzo za Disemba huenda zikatawaliwa na vinara hao wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’